[ad_1]
Na GEOFFREY ANENE
MKENYA Johanna Omolo yuko katika orodha ya wanasoka tisa ambao wameagana kwaheri na BB Erzurumspor baada ya klabu hiyo kutemwa kutoka Ligi Kuu ya Uturuki.
Vyombo vya habari nchini humo vimetaja wachezaji wengine walioondolewa kikosini kuwa Arvydas Novikovas, Petrus Boumal and Adolphe Teikeu, Jakub Szumski, Elba Rashani, Leo Schwechlen, Zakarya Bergdich na Brahim Darri.
“Wachezaji hawa walijiunga na BB Erzurumspor msimu huu kwa kandarasi iliyokuwa na makubaliano kuwa watakuwa huru kujiunga na klabu nyingine Erzurumspor ikitemwa,” taarifa hizo zinasema.
Erzurumspor pia imekatiza kandarasi za wachezaji Mitchell Donald, Arturo Mina, Fabien Farnolle, Armando Sadiku, Aatif Chahechouhe, Mostapha El Kabir, Yaw Ackah na Manuel da Costa.
Omolo,31, alijiunga na Erzurumspor mnamo Januari 14 mwaka huu akitokea Cercle Brugge inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Kandarasi yake inatarajiwa kukatika rasmi mwezi huu mnamo Juni 30. Erzurumspor ilikamilisha Ligi Kuu katika nafasi ya 18 kwa alama 40. Ilitemwa pamoja na Ankaragucu na Genclerbirligi (alama 38) na Denizlispor (28).
Omolo ameishi nchini Ubelgiji kwa miaka 14 na ana uraia wa taifa hilo.
[ad_2]
Source link