Home » Wacheni Uchokozi! Wanamtandao Wamlima Ngunjiri Wambugu Baada ya Selfie na Omanga ▷ Kenya News
News

Wacheni Uchokozi! Wanamtandao Wamlima Ngunjiri Wambugu Baada ya Selfie na Omanga ▷ Kenya News

[ad_1]

Mbunge wa Nyeri Mjini Wambugu Ngunjiri alijipata pabaya mtandaoni baada ya kulimwa alipopiga picha na wanasiasa wenzake Catherine Waruguru na Millicent Omanga.

Wacheni Uchokozi! Wanamtandao Wamlima Ngunjiri Wambugu Baada ya Selfie na Omanga
Wanamtandao Wamlima Ngunjiri Wambugu Baada ya selfie na Millicent Omanga na Cate Waruguru. Picha: Millicent Omanga
Source: Facebook

Picha hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao na Omanga, ilizua hisia mseto huku wakosoaji wa Ngunjiri wakishangaa ni vipi alifurahia kupenyezwa kwenye selfie ya vipusa.

Ngunjiri amekuwa akirushiwa mishale ya kisiasa huku akidai kuwa na ‘mehemehe’ za kisiasa kama kina dada kwenye saluni.

Hatua yake ya kupiga selfie na kina dada hao iliwapa wakosoaji nafasi ya kutia muhuri madai yao na kusema ana ‘umama sana’.

Habari Nyingine: DP Ruto Asisimka Baada ya Rais wa Marekani Kuhubiri Injili ya Wheelbarrow

Msemeo huo hutumika mtandaoni kuwatania wale ambao wana hulka kama za baadhi ya kina dada kama kasheshe nyingi.

Huu hapa utani wa wanamtandao kwa mbunge huyo

Source: Tuko News



[ad_2]
Source link