Home » Afisa wa Jeshi la Wanamaji Azirai Wakati wa Sherehe za Madaraka Dei ▷ Kenya News
News

Afisa wa Jeshi la Wanamaji Azirai Wakati wa Sherehe za Madaraka Dei ▷ Kenya News

[ad_1]

– Afisa huyo wa Jeshi la Wanamaji alizimia akiwa kazini mnamo Jumanne, Juni 1 katika Uwanja wa Jomo Kenyatta Kisumu

– Alisaidiwa na maafisa wa Msalaba Mwekundu ambao walimpeleka kupokea matibabu

– Jukumu la Kikosi cha Wanamaji kimetwikwa jukumu la kulinda taifa dhidi ya tishio la mashambulizi ya baharini

Afisa wa Jeshi la Wanamaji alizimia wakati wa sherehe za Madaraka Dei zilizoandaliwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Kisumu mnamo Jumanne, Juni 1.

Afisa huyo alikuwa katika kikosi cha Maafisa wa Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanahewa na Kikosi cha Ulinzi.

Habari Nyingine: Polisi Embakasi Amuua Mwanaume Baada ya Kuzozanania Penzi

Afisa wa Jeshi la Wanamaji Azirai Wakati wa Sherehe za Madaraka Dei
Maafisa wa ulinzi wa Kenya wakati wa gwaride. Picha: KDF.
Source: Facebook

Katika picha zilizosambaa mitandaoni, maafisa wawili walionekana wakimsaidia mwenzao ambaye alikuwa akiugua.

Walimbeba na kumpeleka kupokea matibabu.

Kwa kawaida, maafisa hujipanga kupamba sherehe hizo kwa kuandaa gwaride la kiheshima.

Baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuwasili katika eneo la sherehe, alikagua gwaride kisha Jeshi la Wanahewa wanawatumbuiza wananchi kwa kuonesha umahiri wao wa kupaa angani wakitumia ndege za kivita.

Habari Nyingine: Aliyekuwa Gavana wa Wajir Mohamed Mohamud Miongoni mwa Wageni Wanaohudhuria Madaraka Day

Vile vile mwanajeshi KDF kutoka kikosi maalum cha parachuti alipata majeraha alipokuwa akitua katika uwanja uo huo wakati wa maadhimisho ya Madaraka.

Afisa huyo alikuwa kati ya wale walioonyesha ustadi wao mbele ya Rais Uhuru Kenyatta, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Naibu Rais William Ruto, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na zaidi ya wageni 3,000 katika ukumbi huo.

Alihudhuriwa na timu ya madaktari katika eneo la tukio kabla ya kuchukuliwa na ambulensi ya jeshi kwa matibabu zaidi.

Habari Nyingine: Mganga Akamatwa Baada ya Kumtepeli Meneja wa Tala Ksh 9 Milioni

Wakati wa hafla hiyo ya kihistoria, maafisa wa kike wa KDF waliotambuliwa kama Kapteni Orina na Kapteni Mutua walipeperusha mabango yaliyokuwa na maudhui ya ‘Mungu ibariki Kenya’.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Source: Tuko.co.ke

[ad_2]
Source link