[ad_1]
Na WYCLIFFE NYABERI
KARIBU watahiniwa wote walipata alama ya ‘E’ katika masomo ya sayansi kwenye shule moja Kaunti ya Kisii.
Watahiniwa 28 wa shule ya upili ya Rianyanchabera walipata alama ya E katika masomo ya Hisabati, Bayolojia na Kemia kwenye Mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE) ambao matokeo yake yalitangazwa Jumatatu.
Ni watahiniwa wawili tu ambao walifanikiwa kupata alama ya D- kwenye masomo hayo.Watahiniwa wanne waliongoza katika shule hiyo, iliyoko katika eneobunge la Bomachoge Borabu, baada ya kupata wastani wa alama ya D.
Wengine 20 walifuatia kwa alama ya D- huku sita wakipata alama ya E. Katika eneobunge jirani la Nyaribari Chache, shule ya upili ya Boronyi haikuwa na sababu ya kusherekea.
Kati ya watahiniwa 22, tisa walipata alama ya D na 12 wengine wakaandikisha gredi za D-. Mwanafunzi mmoja aliandikisha alama ya E.Tulipotembelea shule hizo, makaribisho hayakuwa mazuri hata kidogo.
[ad_2]
Source link