Home » Arsenal yakataa wazo la Newscastle United kutaka kumsajili Joe Willock kwa mkataba wa kudumu – Taifa Leo
News

Arsenal yakataa wazo la Newscastle United kutaka kumsajili Joe Willock kwa mkataba wa kudumu – Taifa Leo

[ad_1]

Na MASHIRIKA

KOCHA Mikel Arteta amesema kwamba kiungo mvamizi Joe Willock atarejea uwanjani Emirates mwishoni mwa msimu huu na kuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Arsenal kwenye kampeni za muhula ujao wa 2021-22.

Sogora huyo raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 amejivunia ufufuo mkubwa wa makali yake kambini mwa Newcastle United waliomsajili kwa mkopo mnamo Januari 2021.

Kufikia sasa, amewafungia kikosi hicho cha kocha Steve Bruce jumla ya mabao saba kutokana na mechi 10.

Mpango wa Arteta kumhusu Willock unafichuka siku chache baada ya Bruce kufichua kwamba angependa kushawishi usimamizi wa Newcastle kumpa Willock mkataba wa kudumu uwanjani St James’ Park.

“Hatuna mpango wowote wa kumtia Willock mnadani au kumtuma kwingineko kwa mkopo muhula ujao. Tunatazamia hali ambapo atarejea kikosini mwishoni mwa msimu huu na kupigania nafasi yake muhula ujao,” akasema Arteta ambaye ni raia wa Uhispania.

“Nafurahia kwamba mambo yanamwendea vizuri. Anazidi kupata tajriba na mechi ambazo amepiga kambini mwa Newcastle zimefichua mengi kuhusu ukubwa wa uwezo wake na nafasi nzuri anayostahili kuchezea uwanjani,” akaongeza Arteta.

Willock ambaye mkataba wake ugani Emirates unatamatika rasmi mnamo 2023, alifungia Arsenal mabao matatu katika Europa League msimu huu kabla ya kuyoyomea Newcastle United.

Katika mchuano wake wa kwanza kambini mwa Newcastle, alifunga bao katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton mnamo Februari kabla ya kupachika wavuni magoli zaidi katika mechi sita zilizopita.

Alichangia pakubwa kuhakikisha kwamba Newcastle almaarufu ‘The Magpies’ wanasalia katika kampeni za EPL muhula ujao. Willock amekuwa mchezaji wa Arsenal tangu akiwa na umri wa miaka minne.

Bao alilowafungia Newcastle dhidi ya Sheffield United mnamo Mei 19 ugani St James’ Park lilimfanya kuvunja rekodi ya Romelu Lukaku (2015) na kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwahi kutikisa nyavu za wapinzani katika mechi sita za EPL mfululizo. Ndiye mchezaji wa tatu wa Newcastle kufanya hivyo baada ya Papiss Cisse (2012) na Alan Shearer (1996).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link