[ad_1]
Na BENSON MATHEKA
SERIKALI itatumia Sh14. 5 bilioni kati ya Sh121 bilioni zilizotengewa Wizara ya Afya katika bajeti ya mwaka 2021/ 2022 kununua chanjo ya corona, Waziri wa Fedha, Ukur Yatani alieleza jana.
Pesa hizo ni kando na Sh3.9 bilioni ambazo serikali itatumia kufanikisha chanjo hiyo kwa Wakenya katika mwaka wa kifedha utakaoanza Julai mwaka huu.Bw Yatani pia alisema kwamba serikali imetenga Sh47.7 bilioni kwa Mpango wa Afya kwa Wote (UHC) ambao ni moja ya Ajenda Nne Kuu za serikali ya Jubilee, ambazo alisisitiza kuwa serikali imejitolea kufanikisha.
Serikali pia imetenga Sh8.7 bilioni kwa shughuli za dharura za kukabiliana na corona na Sh5.8 bilioni za kukabiliana na Malaria.Kwenye bajeti aliyosoma bungeni jana, Bw Yatani alisema serikali imetenga Sh450 milioni kuanzisha kituo cha kutibu saratani katika hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta na Sh350 milioni kuanzisha vituo sawa katika kaunti za Meru na Kakamega.
Katika bajeti hiyo, Bw Yatani alifichua kwamba serikali imetenga Sh7.2 bilioni za kununua vifaa vya matibabu na Sh8 bilioni kutoa bima ya afya kwa watu wasiojiweza katika jamii wakiwemo wazee.Katika mwaka wa kifedha ujao, serikali itatumia Sh4.1 bilioni kufadhili huduma za akina mama kujifungua bila malipo.
[ad_2]
Source link