Home » Chelsea kutumia Abraham na Kepa kushawishi Spurs kuwapa fowadi Harry Kane – Taifa Leo
News

Chelsea kutumia Abraham na Kepa kushawishi Spurs kuwapa fowadi Harry Kane – Taifa Leo

[ad_1]

Na MASHIRIKA

CHELSEA wako radhi kuwapa Tottenham fowadi Tammy Abraham na kipa Kepa Arrizabalaga pamoja na kitita cha Sh8 bilioni ili kumpata fowadi Harry Kane ambaye amefichua azma ya kuagana rasmi na waajiri wake msimu huu.

Chelsea ndicho kikosi cha hivi karibuni kujitosa kwenye vita vya kuwania maarifa ya Kane ambaye pia anahemewa pakubwa na Manchester United, Manchester City, Barcelona na Real Madrid.

Hata hivyo, mwenyekiti Daniel Levy amesisitiza kwamba Spurs hawana mpango wowote wa kumwachilia Kane hivi karibuni na iwapo watalazimika kumtia mndani basi hawana nia ya kumruhusu nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kujiunga na kikosi chochote cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Isitoshe, huenda ikawa vigumu kwa Spurs kukubali ofa hiyo ya Chelsea baada ya Levy, ambaye amefichua mpango wa kukutana na Kane moja kwa moja, kusisitiza kwamba bei ya mwanasoka huyo raia wa Uingereza kwa sasa ni Sh21 bilioni.

Uhusiano kati ya Chelsea na Spurs katika soko la uhamisho na usajili wa wachezaji haujakuwa mzuri tangu Spurs wazime maazimio ya Chelsea kumsajili kiungo Luka Modric mnamo 2011. Mwaka mmoja baadaye, Chelsea nao walizima ndoto za Spurs kujinyakulia huduma za Willian Borges ambaye kwa sasa anachezea Arsenal.

Kwa mujibu wa Chelsea, Abraham kwa sasa hana uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza cha kocha Thomas Tuchel ambaye amesalia kutegemea pakubwa mafowadi Timo Werner, Hakim Ziyech na Christian Pulisic.

Chelsea wamefichua kwamba bei ya Abraham ni Sh5.6 bilioni. Hata hivyo, huenda bei hiyo ikashuka zaidi ikizingatiwa kwamba thamani hiyo ilitolewa kwa kutathmini mchango wa fowadi huyo raia wa Uingereza kambini mwa Chelsea kati ya Agosti 2019 na Machi 2020. Katika kipindi hicho, Abraham alifungia waajiri wake mabao 15 kutokana na mechi 22.

Licha ya Arrizabalaga kusajiliwa kwa kima cha Sh10 bilioni kutoka Athletic Bilbao mnamo 2018, makali ya kipa huyo yalishuka pakubwa ugani Stamford Bridge kiasi cha Chelsea kulazimika kumsajili mlinda-lango Edouard Mendy ambaye kwa sasa ni chaguo la kwanza.

Arrizabalaga amechezea Chelsea mara 13 katika mashindano yote ya msimu huu.

Chelsea ambao pia wamefichua azma ya kumwachilia fowadi Callum Hudson-Odoi, 20, kuyoyomea Bayern Munich msimu huu, wanawania pia maarifa ya Erlinga Haaland wa Borussia Dortmund na Romelu Lukaku wa Inter Milan. Hudson-Odoi amewajibishwa na Chelsea mara 10 pekee katika mapambano yote ya muhula huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]
Source link