[ad_1]
Wakazi wa Kisumu Jumanne Juni 1 alipokelewa kwa shangwe na wakazi wa Kondele baada ya sherehe za Madaraka Dei.
Video ya msafara wa DP ukipokewa na wakazi hao waliotaka awahutubie imesambaa kwenye mtandao.
Ruto alikuwa kwenye msafara wake pekee baada ya Rais Uhuru Kenyatta na wageni wake kuenda kivyao.
Wakazi hao walionekana kumpa upendo mkubwa licha ya kuwa hiyo ni ngome ya kinara wa ODM Raila Odinga.
Wandani wa DP walianza sherehe kwa mapokezi hayo huku Mbunge Oscar Sudi akisema mahasimu wa Ruto wataingiwa na kinyongo.
Habari Nyingine: Usalama wa Rais: Jamaa Ajaribu Kumkaribia Uhuru Jukwaani Akihutubia Taifa
“Mtaanza kuskia sasa wakisema kuwa haya mapokezi yalipangwa. Tunawaheshimu sana nyinyi watu wa Luo Nyanza. Wakati wa Mungu ndio wakati unaofaa,” Sudi alisem.
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro aliruka kwenye mtandao pia na kusifu wakazi wa Kisumu kwa kumpa DP heshima kubwa.
“Asanteni Hustlers wa Kisumu. Nyinyi ni ishara ya Kenya inapoelekea. Tunaheshimu viongozi wote lakini Ruto ndio kiongozi wetu 2022. Hustlers hawana kabila na wanajua nani watampigia kura,” aliandika Nyoro.
Habari Nyingine: Afisa wa Jeshi la Wanamaji Azirai Wakati wa Sherehe za Madaraka Dei
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari kemekem za TUKO hapa
Source: Tuko.co.ke
[ad_2]
Source link