[ad_1]
Na VALENTINE OBARA
WAKILI Paul Gicheru ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutupilia mbali ushahidi ambao unatarajiwa kutumiwa na upande wa mashtaka dhidi yake, akidai kwa kuwa hauna msingi.
Bw Gicheru anakabiliwa na mashtaka kuhusu madai ya kushawishi mashahidi wajiondoe katika kesi iliyokuwa ikimwandama Naibu Rais William Ruto kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007.
Kupitia kwa wakili wake Michael Karnavas, Bw Gicheru alifananisha upande wa mashtaka katika ICC unaoongozwa na Bi Fatou Bensouda, na mchawi katika hadithi ya kale ya ‘Wizard of Oz’ ambaye alikuwa na sura ya kutisha ilhali kikweli, hakuwa na nguvu zozote za kuridhisha.
“Sawa na jinsi pazia ilifunguliwa katika hadithi ya ‘Wizard of Oz’ na mchawi aliyeogopwa sana akabainika kuwa mwanamume mwoga, tunapoondoa pazia katika kesi iliyowasilishwa na upande wa mashtaka tunabainisha kuna lengo la kupotosha mahakama izingatie ushahidi wa uongo usio na msingi kuendeleza kesi mbele,” akasema katika nakala iliyowasilishwa mahakamani.
Kulingana na Bw Karnavas, ushahidi kama vile rekodi za sauti ambazo Bi Bensouda anategemea hazifai kukubaliwa kwa vile hakuna thibitisho lolote kuhusu watu walionaswa wakizungumza kuhusu njama za kuvuruga mashahidi wa kesi ya Dkt Ruto.
Bi Bensouda alikuwa ameambia mahakama kwamba kesi dhidi ya Bw Gicheru inafaa kuendelea mbele kwa vile kuna ushahidi wa kutosha utakaothibitisha alihusika katika njama hizo kwa ushirikiano na watu wengine ambao hawajakamatwa.
[ad_2]
Source link