[ad_1]
– Kabogo alitaka Rais Uhuru apashwe habari kuwa katiba haimruhusu kuendelea kuhudumu kwa kipindi kingine
– Kumekuwa na madai kutoka kwa wakosoaji wa Rais kuwa kuna mpango wa kuendeleza kipindi cha serikali yake
– Kabogo alisema yuko tayari kuchukua usukani wa kuongoza jamii ya mt Kenya ambayo inabaki yatima Uhuru akiondoka
Siasa za Mt Kenya zinaendelea kutokota huku Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kustaafu ifkapo mwaka wa 2022.
Vigogo kadhaa kutoka eneo hilo wamekuwa wakijipanga kuchukua usukani kuongoza jamii ya eneo hilo ambayo imekuwa chini ya Kenyatta kama msemaji wao tangu 2013.
Aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo amesema yuko tayari kuvaa viatu vya Uhuru baada yake kustaafu.
“Rais Kenyatta anaenda nyumbani na hapo hakuna mjadala, kama anataka kuendelea ajue hilo haliwezekani,” alisema Kabogo.
Habari Nyingine: “Punguza Bangi” Khalighraph Amjibu Bahati Baada ya Kutunga Wimbo wa Kumchongoa
“Kama kuna mtu wao hapa amfikishie huo ujumbe, ile katiba tuko nayo haiwezi kuruhusu hilo, inasema aweze nyumbani,” aliongeza mwanasiasa huyo mwenye mifuko mizito
Kabogo alionekana kupuuza kutawazwa kwa Spika wa bunge Justin Muturi kuwa msemaji kwa jamii ya Mt Kenya.
Alisema kila eneo linafaa kuwa na kiongozi wao na wala si watu kutoka nje akitaka wazee wa Gikuyu kuwa makini na wanavyowatawaza viongozi.
Habari Nyingine: Rais wa Ghana Amuomba Nyota wa Chelsea Hudson-Odoi Abadilishe Uraia
“Hatuwezi kuletewa kiongozi. Kila watu wajibebe hapa kubebwa na wengine. Hatuwezi kukubali, hiyo nafasi Rais Uhuru anashikilia mimi ndio nitachukua,” alisema.
Muturi alitawazwa na kisha akatangaza kuwa anawania urais ifikapo 2022 na kutaka eneo la Mt Kenyatta Magharibi kumuunga mkono.
Alisema Mt Kenya Mashariki, ambao ni Embu na Meru, wamekuwa wakiunga mkono wenzao wa kutoka Kiambu na Nyeri na hivyo ni wakati wa kulipa deni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habario kemkem za TUKO hapa
Source: Kenya Breaking News Today
[ad_2]
Source link