[ad_1]
Na MARGARET MAINA
NDIZI za plantains zikikaangwa huwa ni tamu na hupendwa sana na raia wa mataifa ya Afrika Magharibi na Walatino.
Unaweza kuandaa plantains ziliwe kwa mchele, maharagwe, kitoweo, au hivyo pekee.
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa mapishi: Dakika 10
Walaji: 4
Vinavyohitajika
– Plantains 10
– Chumvi
– Mafuta ya kupikia
Maelekezo

Osha ndizi kisha chambua na ukatekate plantains zako.
Nyunyuzia chumvi pande zote mbili.
Kisha weka kikaangio mekoni na uweke mafuta ya kupikia.
Ongeza plantains na kaanga upande mmoja hadi ziwe na rangi ya hudhurungi, kisha ugeuze na kukaanga upande mwingine.
Epua plantains zako kwa uangalifu kutoka kwa mafuta moto kwa kutumia kijiko.
Ziweke kwenye tissue za jikoni ili mafuta yachujike kabisa.
Rudia kukaanga plantains zilizobakia mpaka zote ziishe.
Pakua na ufurahie.
[ad_2]
Source link