Home » Jinsi ya kuandaa plantains – Taifa Leo
News

Jinsi ya kuandaa plantains – Taifa Leo

[ad_1]

Na MARGARET MAINA

[email protected]

NDIZI za plantains zikikaangwa huwa ni tamu na hupendwa sana na raia wa mataifa ya Afrika Magharibi na Walatino.

Unaweza kuandaa plantains ziliwe kwa mchele, maharagwe, kitoweo, au hivyo pekee.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 4

Vinavyohitajika

– Plantains 10

– Chumvi

– Mafuta ya kupikia

Maelekezo

Jinsi ya kuandaa plantains – Taifa Leo
Ndizi aina ya plantains. Picha/ Margaret Maina

Osha ndizi kisha chambua na ukatekate plantains zako.

Nyunyuzia chumvi pande zote mbili.

Kisha weka kikaangio mekoni na uweke mafuta ya kupikia.

Ongeza plantains na kaanga upande mmoja hadi ziwe na rangi ya hudhurungi, kisha ugeuze na kukaanga upande mwingine.

Epua plantains zako kwa uangalifu kutoka kwa mafuta moto kwa kutumia kijiko.

Ziweke kwenye tissue za jikoni ili mafuta yachujike kabisa.

Rudia kukaanga plantains zilizobakia mpaka zote ziishe.

Pakua na ufurahie.

[ad_2]
Source link