Home » Leicester wakomoa Man-United na kushindia Man-City taji la EPL – Taifa Leo
News

Leicester wakomoa Man-United na kushindia Man-City taji la EPL – Taifa Leo

[ad_1]

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City walitwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya tatu chini ya kipindi cha misimu minne baada ya Leicester City kuvuna ushindi wao wa kwanza uwanjani Old Trafford tangu 1998 katika mchuano uliowakutanisha na Manchester United, Jumanne.

Ushindi huo wa Leicester uliweka hai ndoto zao za kukamilisha kampeni za muhula huu ndani ya orodha ya nne-bora na hatimaye kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao wa 2021-22.

Kushindwa kwa Man-United kunamaanisha kwamba sasa ni pengo la pointi 10 ndilo linatamalaki kati yao na Man-City huku zikiwa zimesalia mechi tatu pekee kwa kampeni za msimu huu kutamatika rasmi.

Bao la kichwa kutoka kwa beki Caglar Soyuncu katika dakika ya 66 lilitosha kumvunia kocha Brendan Rodgers wa Leicester tabasamu huku goli hilo likiendeleza ubabe wa Man-City katika soka ya Uingereza chini ya kocha Pep Guardiola aliyeajiriwa na Man-City mnamo 2016-17 kutoka Bayern Munich.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Man-United alikifanyia kikosi alichokitegemea dhidi ya Aston Villa mnamo Mei 9 mabadiliko 10. Chipukizi Mason Greenwood alisawazishia  Man-United katika dakika ya 15, dakika tano baada ya kinda Luke Thomas, 19, kuwaweka Leicester kifua mbele.

Matokeo hayo yalikomesha rekodi ya kutoshindwa kwa Man-United katika jumla ya mechi 14 za EPL kwa mfululizo tangu walipopigwa na Sheffield United uwanjani Old Trafford mnamo Januari 27, 2021.

Leicester kwa sasa wanahitaji alama nne pekee kutokana na mechi mbili zilizosalia msimu huu dhidi ya Chelsea na Tottenham Hotspur ili kukamilisha kampeni za EPL msimu huu ndani ya orodha ya nne-bora.

Kabla ya hapo, masogora hao wa kocha Rodgers watapania kutia kapuni Kombe la FA kwa mara ya kwanza katika historia watakapovaana na Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA itakayowakutanisha ugani Wembley mnamo Mei 15, 2021.

Leicester walijibwaga ugani wakitawaliwa na kiu ya kukomesha rekodi mbovu dhidi ya Man-United ikizingatiwa kwamba walikuwa wameshinda mechi mbili pekee kutokana na 29 za awali katika EPL. Leicester walikuwa pia wameshinda mchuano mmoja pekee kati ya 22 iliyowahi kuwakutanisha na Man-United ligini katika uga wa Old Trafford.

Baada ya kuchuana na Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA mnamo Jumamosi ijayo, Leicester wamepangiwa kuvaana tena na masogora hao wa kocha Thomas Tuchel uwanjani Stamford Bridge mnamo Mei 18, 2021. Man-United kwa upande wao watakuwa wenyeji wa Liverpool ligini mnamo Mei 13, 2021 uwanjani Old Trafford.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]
Source link