Home » Mageuzi yaja kwa viongozi wasaliti na wenye ubinafsi – Taifa Leo
News

Mageuzi yaja kwa viongozi wasaliti na wenye ubinafsi – Taifa Leo

[ad_1]

Na WANDERI KAMAU

MUNGU alitumia maandishi mene mene tekel upharsin kwa Mfalme Nebchadnezzar wa Babylon kumwambia ufalme wake ulikuwa umefika mwisho.

Simulizi kumhusu Mfalme Nebchadnezzar ni miongoni mwa zile zenye umaarufu mkubwa kwenye Biblia na vitabu vingine vya kidini.

Mungu alikasirishwa na mfalme huyo kwa kuruhusu kila aina ya maovu kuenea katika falme yake, kiasi cha wenyeji kumsahau.

Wenyeji waliabudu sanamu kama miungu wao, badala ya kumheshimu na kumwogopa Mwenyezi Mungu.

Kilichomkasirisha Mungu zaidi ni dhuluma za mfalme huyo dhidi ya watu ambao walijitokeza kuwa wanaotetea ukweli na maadili mema.

Bila kuogopa, alikuwa akiamuru wachomwe ama warushwe kwenye jumba moja alikokuwa amewafuga mbwa na simba maalum kumshambulia yeyote ambaye angepatikana akimwabudu Mungu badala ya sanamu alizokuwa ameweka kila mahali.

Hata hivyo, Mungu alisikia vilio vya watu wake na kumpa adhabu kali kiongozi huyo, ambayo hutumika kama mfano katika majukwaa ya usomi wa Dini, Falsafa, Fasihi, Sayansi ya Siasa na Historia.

Mungu alimgeuza mfalme huyo kuwa mnyama, ambapo alikula nyasi msituni kwa muda wa miaka saba.

Bila shaka, kabla ya adhabu hiyo, Mfalme Nebchadnezzar alikuwa amepewa onyo kali na manabii kwamba Mungu alikuwa akipanga kumwadhibu kwa kuruhusu maovu kuenea bila kuchukua hatua zozote.

Simulizi hii inarejelea hali ilivyo nchini, barani Afrika na duniani kote kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaopania kuendelea kuyaongoza mataifa yao.

Ni ujumbe mzito.

Hapa nchini, huu ni ujumbe fiche kwa vigogo wa kisiasa ambao wamekuwa wakiendelea kukwamilia mamlakani kuwa kuna wimbi la mageuzi makubwa linalowadia.

Ni wimbi kubwa na hatari. Halitakuwa na huruma. Litaendeshwa na raia wenyewe na watu wa kawaida.

Ndani yake mtakuwemo na sauti ya Mungu. Ni sauti ya kipekee yenye uchungu na itakayowaongoza raia kuwaondoa viongozi na wanasiasa hao. Wimbi hilo litawaongoza raia kama vile Mungu alitoa mwenge maalum kuwaongoza Waisraeli walipokuwa jangwani kuwapa mwongozo.

Kwa wakati huu, ‘Waisraeli’ ni vijana, wanawake na makundi mengine katika jamii yaliyotengwa na kusahaulika. Ni wazi kuwa tangu tulipojinyakulia uhuru, vijana nchini wamegeuka kuwa mateka wa wanasiasa kila uchaguzi mkuu unapowadia.

Ilivyo sasa, hali ni mbaya nchini. Watu wengi wamepoteza matumaini maishani kutokana na ugumu wa gharama ya maisha na ukosefu wa ajira.

Hii ni licha yao kuwa na masomo ya kiwango cha juu!

Tukio lilodhihirisha kiwango cha ukosefu wa ajira nchini ni idadi ya watu waliotuma maombi ya kutaka kuwa makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Ingawa tume ilitangaza nafasi nne pekee, zaidi ya watu 600 walituma maombi yao, huku 137 kati yao wakiwa na shahada za uzamifu!

Maswali yanayoibuka ni: Nafasi za watoto wetu walio katika shule za upili na vyuo vikuu zi wapi? Mustakabali wao utakuwa vipi?

Kinaya ni kuwa, viongozi wanaonekana kutojali hata kidogo. Badala yake, wameelekeza juhudi zao zote kwa abrakadabra za Mpango wa Maridhiano (BBI) na ushindani wa kisiasa usiofaa.

[ad_2]
Source link