Home » Mechi za Betway Cup kuchacha – Taifa Leo
News

Mechi za Betway Cup kuchacha – Taifa Leo

[ad_1]

Na JOHN ASHIHUNDU

Michuano ya Betway Cup raundi ya 32 bora zitachezwa leo na kesho katika viwanja mbali mbali kote nchini.

Katika mechi za leo Jumamme, AFC Leopards ambao majuzi walichapwa 3-1 na Bidco United katika pambano la ligi kuu ya Kenya (FKF-PL) wamepangiwa kukutana na Posta Rangers jijini Nairobi, wakati Bandari FC wakiwakiwaalika Dimba Patriots ugani Mbaraki kuanzia saa tisa alasiri.

Washindi kwenye raundi hii watafuzu kwa raundi ya 16 bora ambayo mechi zake zitachezwa Jumamosi na Jumapili.

Timu zitakazobakia mashindanoni zitatinga raundi ya robo-fainali ambayo mechi zake zitachezwa Juni 9 na Juni 10, huku nusu-fainali ikipangwa kufanyika Juni 12 na Juni 13.

Gor Mahia ambao waliwabwaga Congo Boys katika raundi ya 64 watakuwa nyumbani ugani Utalii kupambana na CUSCO FC Alhamisi, wakati Kariobangi Sharks wakiwaalika Tandaza FC uwanjani humo hapo kesho.

Ulinzi Stars watasafiri hadi Wundanyi kupepetana na Sofapaka katika uwanja wa Dowson Mwanyumba.

Kwingineko, leo alasiri Nation FC watakuwa Magharibi mwa Kenya kucheza na Bungoma Superstars. Mechi hiyo itachezewa Sudi Stadium kuanzia saa nane.

Bungoma wanawekewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo kutokana na ufanisi wao mkubwa katika mechi za Daraja la Kwanza, Kanda B, lakini hawatarajii kazi rahisi dhidi ya vijana wa Nation ambao wamekuwa katika mazoezi makali kwa wiki mbili.

Wakufunzi wa Nation FC walikamlisha mazoezi yao jana chini ya uangalifu mkubwa wa amkocha Augustine Kuta na John Wahome katika uwanja wao wa St Mary’s School kwa ajili ya mechi ya kesho.

Meneja wa Nation FC Elias Makori, anayeomboleza kifo cha babake mzazi Samuel Obanyi aliyefariki wiki moja iliyopita, pia alihudhuria mazoezi ya Jumatatu.

Mzee Obanyi atazikwa Ijumaa nyumbani kwake Kebirigo, Kaunti ya Nyamira.

Bungoma Superstars, chini ya ukufunzi wa Erick Wasike, wataingia uwanjani baada ya majhuzi kuandikisha ushindi dhidi ya GDC katika mechi yao ya ligi iliyochezewa Airstrip Ground mjini Bungoma.

Wenyeji watamtegemea Herbert Waswa – aliyefunga bao la ushindi dhidi ya GDC- akishirikiana na Bokings Odero, Abel Wafula, Dan Juma, Kennedy Oloo na Anthony Ochieng.

Nation FC walifuzu kwa raundi hii baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Vihiga Sportiff katika raundi ya 64 ugani Mumboha mwezi Februari.

Makori aliishukuru Nation Media Group chini ya Afrisa Mkuu, Stephen Gitagama kwa kuendelea kuiunga mkono timu hiyo, licha ya changamoto za Covid-19.

Ratiba ya FKF Raundi ya 32:

Leo (Jumanne): Mara Sugar na NYSA (Green Stadium, Awendo) saa nane;

Egerton na Administration Police (Egerton University) saa nane;

Malindi Progressive na Luanda Villa (Alaskan, Malindi) saa nane;

Bandari na Dimba Patriots (Mbaraki, Mombasa) saa tisa;

Marafiki na Tusker (Kinungu Stadium, Nyeri) saa tisa;

Kajiado North na Sigalagala TTI (GEMS Cambride, Nairobi) saa saba;

KCB na Transfoc (GEMS Cambride, Nairobi) saa tisa;

Bungoma Superstars na Nation FC (Sudi Stadium, Bungoma) saa nane;

Fortune Sacco na Nairobi City Stars (Kianyaga grounds, Kerugoya) saa nane;

Twomoc na Vegpro (Nakuru ASK grounds) saa nane;

Equity na Keroka TTI (Thika Stadium) saa saba;

Bidco United na Tywford (Thika Stadium) saa tisa;

AFC Leopards na Posta Rangers (Kasarani) saa tisa.

Kesho (Jumatano):

Gor Mahia na CUSCO (Kasarani) saa tisa;

Kariobangi Sharks na Tandaza (Utalii, Nairobi) saa tisa;

Sofapaka na Ulinzi Stars (Wundanyi Stadium, Taita Taveta) saa tisa.

[ad_2]

Source link