Home » Mimi Sina Pesa Lakini Maono, Seneta Malala Kuwania Kiti cha Ugavana wa Kakamega ▷ Kenya News
News

Mimi Sina Pesa Lakini Maono, Seneta Malala Kuwania Kiti cha Ugavana wa Kakamega ▷ Kenya News

[ad_1]

Seneta Malala ametangaza kwamba atawania kiti cha ugavana wa kaunti ya Kakamega mwaka wa 2022

– Malala alisema ingawa hana pesa lakini ana maono kwa wakazi wa kaunti hiyo

– Seneta huyo amefutilia mbali madai kwamba amekuwa akiwafurahisha wakazi na bidhaa kadhaa wa kadhaa ikiwa ni mojawapo wa njia ya kujipigia debe

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ametangaza kwamba ana nia ya kumbandua uongozini Gavana wa sasa wa Kakamega Wycliffe Oparanya katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Habari Nyingine: Nairobi: Kijogoo Afumaniwa Akipakua Asali ya Vidosho Wawili

Mimi Sina Pesa Lakini Maono, Seneta Malala Kuwania Kiti cha Ugavana wa Kakamega
Malala alisema ingawa hana pesa lakini ana maono kwa wakazi wa kaunti hiyo.Picha: Cleophas Malala.
Source: Facebook

Habari Nyingine: Usidanganyike na Ngozi Nyororo, Mwanamke Anayeishi na HIV Awashauri Wakenya

Malala amewaahidi wapinzani wake kwamba kutakuwa na upinzani mkali akidai kwamba ingawa hana pesa lakini ana maono makubwa kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Akizungumza akipeana msaada wa chakula kwa familia zisizojiweza kaunti ya Kakamega Alhamisi, Mei 13 Malala alisema kuwania kiti hicho sio kwa ajili ya manufaa yake ila kwa ya wakazi wa kaunti hiyo.

” Sababu kuu ya kuwania kiti cha ugavana ni kuendelea kuwahudumia wakazi wa Kakamega. Mimi nimekuja na maono, sina pesa. Serikali huwa haitengi fedha za maendeleo kwa maseneta, nimekuwa nikitumia fedha zangu kukabiliana na changamoto ambazo wakazi wa kaunti yangu wanakabiliana nazo,” Alisema Malala.

Malala amekuwa akigonga vicha vya habari kwa sababu kadhaa lakini hajakuwa akikataa tamaa kwa ajili ya kuwapa wananchi hudumu wanayostahili.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Source: Tuko.co.ke

[ad_2]
Source link