Home » Mwanadada alenga shabaha ya juu awe miongoni mwa wasanii mahiri – Taifa Leo
News

Mwanadada alenga shabaha ya juu awe miongoni mwa wasanii mahiri – Taifa Leo

Mwanadada alenga shabaha ya juu awe miongoni mwa wasanii mahiri – Taifa Leo

[ad_1]

Na JOHN KIMWERE

INGAWA hajapiga hatua kubwa anasema amepania kujituma kisabuni ili kuhakikisha ameibuka kuwa miongoni mwa wasanii mahiri katika sekta ya uigizaji duniani.

Alice Njeri Muthoni ni mwanahabari na mwigizaji chipukizi anayepania kufuata nyayo za mwigizaji wa filamu za Hollywood, Priyanka Chopra mzawa wa India aliyejizolea umaarufu kupitia filamu kama ‘Quantico,’ na ‘White Tiger’ kati ya zingine. Kipusa huyu ni mwana habari katika kituo cha Redio cha Bus Radio Sauti ya Kajiado katika Kaunti ya Kajiado.

RIWAYA

Dada huyu ambaye pia kisanaa anafahamika kama Alice kwenye filamu za steji, shoo ambazo huigiza kwa kufuata mwongozo wa vitabu ambavyo wanafunzi hutahiniwa kwavyo setbooks ikiwemo riwaya.

”Maana ninahisi nina kipaji, mwanzo wa ngoma nimepania kujijenga katika uigizaji wa filamu zinazotosha mboga kupeperushwa kwenye runinga za kitaifa. Ingawa bado sijapata mashiko katika tasnia ya filamu nchini uigizaji umekuwa tegemeo langu ndani ya miaka kadhaa iliyopita kabla sijaanza kibarua cha uanahabari mwaka huu 2021,” binti huyu anasema na kuongeza kuwa sekta ya uigizaji imeajiri watu wengi nchini.

Mwanadada alenga shabaha ya juu awe miongoni mwa wasanii mahiri – Taifa Leo
Mwigizaji chipukizi Alice Njeri Muthoni. Picha/ John Kimwere

Mwanadada huyu alianza kujituma katika masuala ya uigizaji mwaka 2012 baada ya kukamilisha elimu ya sekondari. Anajivunia kufanya kazi na makundi kadhaa ikiwamo Jicho 4 Productions, Forever Arts Group na Liquids Art Entertainment.

LUPITA NYONG’O

”Nikiwa mtoto nilitamani kuhitimu kuwa mwanahabari lakini pia mwigizaji ambapo katika tasnia ya maigizo, kazi na ukakamavu wake Lupita Nyong’o Mkenya anayetamba katika filamu za Hollywood vilinitia moyo zaidi,” akasema.

Anaongezea kuwa kujituma kwake kulimzawadi tuzo ya Oscar iliyomtia motisha zaidi. Kadhalika anadokeza kuwa Lupita ameibuka kivutio kikubwa kwa waigizaji wanaokuja hapa nchini.

Chipukizi huyu anajivunia kushiriki filamu moja iitwayo ‘Kihiko'(Harusi) iliyopata mpenyo kupeperushwa kupitia runinga ya mtandaoni kwa jina Thingira TV. Kwa wasanii wa Afrika dada huyu angependa kufanya kazi na waigizaji kama Gennevieve Nnaji wa Nigeria (Blood Sisters,’ ‘Lion Heart). Pia yupo mwigizaji wa Tanzania, Jacqueline Wolper ambaye ameshiriki filamu kama ‘Red Valentine,’ na ‘Family Tears,’ kati ya nyingine.

Mwigizaji chipukizi Alice Njeri Muthoni. Picha/ John Kimwere

KUNOA

”Bila mapendeleo wala kuongeza kachumbari sekta ya filamu hapa Kenya inayo nafasi nzuri kupiga hatua tena zaidi na kufaidi wasanii wengi wanaume kwa wanawake,” akasema na kuongeza kuwa hata hivyo inahitaji kufanyiwa kazi kubwa hasa katika uwekezaji.

Pia anasema kuna umuhimu mkubwa kwa waigizaji chipukizi kutambuliwa na kuanza kunolewa makali yao wakiwa wadogo kama ilivyo katika mataifa yanayoendelea.

Kuhusu masuala ya mahusiano anasema, ”Kwa sasa nipo singo lakini sitaki kuingia katika mahusiano hivi karibuni. Wanaume wamenivunja moyo mara kadhaa ambapo kiasi nimeamua kupiga breki nijijenge kwanza.”

Anahimiza wasanii chipukizi kuwa wasivunjike moyo kwa kukosa ajira mbali wazidi kujituma wanapopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na waamini ipo siku Mungu atafungua milango ya mafanikio.

[ad_2]

Source link