[ad_1]
– Slaida Vugutsa aliondoka nyumbani kwao na kusafiri hadi Saudi Arabia kwa ajili ya kujitafutia ajira Januari 2020
– Familia yake ilisema ilizungumza naye mara ya mwisho Agosti 2020 wakati ambapo matatizo yalikuwa yameanza kumuandamana
– Imeripotiwa kwamba, familia ilifahamishwa kuhusu kifo chake na izara ya Mambo ya Ndani Machi 2021
Familia moja kutoka kaunti ya Kakamega imelazimika kukatiza mipango ya mazishi baada ya mwili wa mpendwa wao kukosa kuwasili nchini kutoka Saudi Arabia.
Slaida Vugutsa ambaye alifariki dunia Aprili, Januari 29 kwa njia ya kutatanisha, inasemekana mwili wake ulisahaulika nchini Ujereumani na ndege ambayo ilikuwa ikiusafirisha.
Familia ya mwendazake iliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumanne Aprili 27 lakini ilishangaa kukosa kuupata mwili wa mpendwa wao.
” Ni jambo la kushangaza kwamba tumesafiri kutoka mkoa wa Magharibi na kufika hapa, tunaambiwa kwamba mwili wa mpendwa wetu haupo, tumearifiwa kwamba mwili wake huenda ulisali Ujerumani., Patrick ambaye ni kakake marehemu alisema.
” Wafanayakazi wa ndege hiyo walionekana kuchanganyikiwa sana walipoulizwa kuhusu mwili wa marehemu, tuliwasikia wakinong’onezea dereva wa gari letu kwamba huendwa waliacha mwili wake nchini Ujerumeni,” Patrick aliongezea.
Partick alifahamishwa baadaye kwamba mwili wa dadake utafikishwa nchini Alhamisi, 29 mwezi huu.
Hata hivyo, dereva wa gari ambalo lilikuwa lisafirishe maiti kutoka Nairobi hadi Kakamega alisisitiza kwamba lazima familia imlipe KSh 40,000 kwa ajili ya kucheleweshwa ikizingatiwa awali alikuwa amelipwa KSh 60,000.
Familia hiyo ambayo tumaini lake la kipekee ni kuuzika mwili wa mpendwa wao, haijaelewa ni kwa nini mwili wake haungefika kwa muda ulioratibiwa.
” Tunashuku kwamba huenda mwili wake haukufika Saudi Arabia, ilikuwa ni njama tu, tuliarifiwa kuhusu kifo chake Machi 22 ilhali alifariki dunia mezi Januari, ” Alisema Talia.
Kwa mujibu wa taarifa kutokaa kwa familia, marehemu ambaye alikuwa na miaka 21 alitoweka nyumbani Januari 2020 na kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutafuta kazi baada ya kukamilisha masomo yake ya shule ya upili.
Dadake alisema Vugutsa alitoweka nyumbani wakati ambapo wazazi walikuwa wanapanga kumpeleka katikia chuo kikuu.
Vugutsa alikuwa kitinda mimba kwa familia yao na alipatikana akiwa amefariki dunia ndani ya kichaka.
.
Source: Tuko Breaking News Latest
[ad_2]
Source link