Home » Nafula aongoza Larissa kunyeshea Asteras AV 10-0 Ligi Kuu ya Wanawake Ugiriki – Taifa Leo
News

Nafula aongoza Larissa kunyeshea Asteras AV 10-0 Ligi Kuu ya Wanawake Ugiriki – Taifa Leo

[ad_1]

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Christine Nafula aliongoza klabu yake ya Larissa kumiminia Agrotikos Asteras AV mabao 10-0 baada ya kutikisa nyavu mara kwenye Ligi Kuu ya soka ya wanawake nchini Ugiriki, Jumapili.

Kiungo huyo Mkenya sasa amefungia Larissa magoli 11 tangu ajiunge na timu hiyo kutoka Dalhem IF nchini Uswidi mwezi Machi.

Mabingwa watetezi PAOK wanaongoza Kundi A ya ligi hiyo kwa alama 24 baada ya kunyeshea Kastoria 14-0 wakishinda mchuano wao wa nane mfululizo.

Larissa, ambayo imepoteza mechi mbili, imerukia nafasi ya pili kutoka nambari nne. Iko alama sita nyuma PAOK nayo Agrotikos Asteras pia ina alama 18 baada ya kujibwaga uwanjani mara saba.

Matokeo (Mei 30): Feidon 2 Ergotelis 1, Elpides Karditsa 2 Trikala 2, Olympiada Ymittos 5 Atromitos 0, Agia Paraskevi 2 Missolonghi 0, Larissa 10 Agrotikos Asteras AV 0, PAOK 14 Kastoria 0, Aris 1 Doxa 1, Gianna 0 Agrotikos Asteras 2.

[ad_2]
Source link