[ad_1]
Na GEOFFREY ANENE
Kamati ya Olimpiki Kenya (NOC-K) ilianza Jumatano mchakato wa kutoa sare za kufanyia mazoezi na za mashindano kwa mashirikisho ya michezo kama sehemu ya kuyasaidia.
Baadhi ya mavazi hayo ni yale yaliyopatikana katika katoni 57 zilizokuwa zimetoweka wakati wea michezo ya Olimpiki 2016 ambayo sasas inafahamika kama sakata ya Rio.
Mashirikisho yaliyopokea mavazi hayo katika siku ya kwanza hapo Januari 27 kusambazia wanamichezo wao ni yale yanayosimamia riadha, mpira wa vikapu, masumbwi, uendeshaji basikeli na gofu. Handboli, mpira wa magongo, raga, uogeleaji, tenisi, tenisi ya meza, voliboli, miereka na unyanyuaji uzani pia yalipokea mavazi hayo.
Alhamisi itakuwa zamu ya mashirikisho yanayosimamia michezo ya ulengaji shabaha, ‘fencing’, judo, karate, mpira wa pete, ‘squash’, ‘softball’, ‘shooting’, taekwondo, ‘triathlon’ na upigaji wa makasia. “Wanamichezo wetu wanahitaji kila msaada wanaostahili wanapojiandaa kwa michezo ya Olimpiki 2021,” kamati hiyo ilisema.
Kenya iliandikisha matokeo yake mazuri zaidi katika Olimpiki jijini Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2016, licha ya wanamichezo kukumbwa na matatizo chungu nzima ikiwemo baadhi yao kukosa jezi hizo za kitaifa.
Mabingwa hao wa Riadha za Dunia 2015 walizoa medali sita za dhahabu, sita za fedha na moja ya shaba wakimaliza katika nafasi ya 15 kati ya mataifa 207 yaliyoshiriki.
[ad_2]
Source link