Home » Tetesi kuhusu ukosefu wa sodo shuleni ni uongo mtupu – Prof Magoha – Taifa Leo
News

Tetesi kuhusu ukosefu wa sodo shuleni ni uongo mtupu – Prof Magoha – Taifa Leo

[ad_1]

Na SAMMY WAWERU

WAZIRI wa Elimu Prof George Magoha amepuuzilia mbali madai ya kuwepo na upungufu wa sodo miongoni mwa wanafunzi shuleni.

Prof Magoha amesema serikali imetoa ufadhili wa kutosha kuhakikisha kila mwanafunzi wa kike anayehitaji vifaa hivyo vya kimsingi, anavipata.

“Tetesi mnazoskia kuhusu kuwepo kwa upungufu wa sodo shuleni ni uongo mtupu. Serikali kila mwaka hutoa kima cha shilingi 490 milioni kuhakikisha kila mwanafunzi anayehitaji anapata,” akasema Waziri.

Prof Magoha alitoa hakikisho hilo Jumatatu, wakati akitangaza rasmi matokeo ya mtihani wa kitaifa kidato cha nne, KCSE 2020.

Sodo ni vifaa vinavyotumika na wanawake wakati wa hedhi. Baadhi ya wanafunzi wameangaziwa kukosa vifaa hivyo muhimu, hususan wanaotoka familia zisizo na uwezo.

Ni hatua inayotajwa kuchangia wanafunzi wa kike kuhadaiwa na wahuni, wakiwaahidi kuwanunulia na hatimaye kuishia kupata mimba za mapema.

[ad_2]

Source link