Home » Wananchi Wauaga Mwili wa Aliyekuwa Kocha wa Raga, Benjamin Ayimba katika Uwanja wa RFUEA ▷ Kenya News
News

Wananchi Wauaga Mwili wa Aliyekuwa Kocha wa Raga, Benjamin Ayimba katika Uwanja wa RFUEA ▷ Kenya News

Wananchi Wauaga Mwili wa Aliyekuwa Kocha wa Raga, Benjamin Ayimba katika Uwanja wa RFUEA ▷ Kenya News

[ad_1]

– Mwili wa Benjamin Ayimba ulifikishwa katika uwanja wa RFUEA Jumatano, Juni 9 kwa wananchi kuutizama na kwa ibada fupi

– Ayimba atazikwa Ijumaa, Juni 11 nyumbani kwake eneo la Alego kaunti ya Siaya

– Aliyekuwa makamo wa Rais Kalonzo Musyoka na maafisa wa chama cha raga nchini waliongoza wananchi katika kumpea mwendazake heshima za mwisho

– Ayimba ambaye alikuwa kocha wa timu ya raga aliaga dunia Ijumaa, Mei 21 akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi

Wananchi walipata fursa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa kigogo wa mchezo wa Raga na pia kocha wa zamani wa timu ya Rugby Sevens, Benjamin Ayimba katika uwanja wa RFUEA siku ya Jumatano, Juni 9.

Habari Nyingine: Makena Njeri Akana Madai Kwamba Michelle Ntalami ni ‘Mkewe’

Wananchi Wauaga Mwili wa Aliyekuwa Kocha wa Raga, Benjamin Ayimba katika Uwanja wa RFUEA
Ayimba atazikwa Ijumaa, Juni 11 nyumbani kwake eneo la Alego kaunti ya Siaya.Picha: Nation.
Source: UGC

Habari Nyingine: Video ya Raila Akisakata Densi Kwenye Klabu Yachangamsha Wanamtandao

Ayimba aliaga dunia Ijumaa Mei 21 akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi, familia ilithibitisha kwamba aliangamizwa na ugonjwa wa Malaria.

Aliyekuwa makamo wa rais Kalonzo Musyoka na maafisa wa chama cha mchezo wa raga nchini walikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria ibada ya wafu kwa mwendazake Ayimba.

Wahubiri Elias Simiyu, Jesse Maina na Purity Murungi waliongoza ibada hiyo huku mwanawe mkubwa wa marehemu Brian akisoma maandiko ya Biblia.

Akimuomboleza babake, Brian aliisihi familia kuwa tulivu na kuzingatia amani wakati huu wa huzuni na majonzi.

Brian pia alichukua fursa hiyo kuwashukuru wahisani, jamaa na marafiki waliosimama nao tangu baba yao alipokuwa mgonjwa hadi kifo chake.

” Asanteni kwa kusimama nasi kwa muda wa miezi mitano iliyopita baba wetu akiwa hospitalini, tunashukuru kwa maombi na misaada ya kifedha,” Brian alisema.

Awali, siku ya Jumanne, Juni 8, ibada nyingine ya wafu kwa mwendazake Ayimba ilifanyika katika kanisa la Our Lady Queen of Peace mtaani South B.

Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa hadi nyumbani kwake eneo la Alego kaunti ya Siaya kwa ajili ya maandalizi ya mazishi siku ya Ijumaa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Source: Tuko Breaking News

[ad_2]
Source link