Home » Wawili wanaswa na noti feki za Sh750 milioni – Taifa Leo
News

Wawili wanaswa na noti feki za Sh750 milioni – Taifa Leo

[ad_1]

WINNIE A ONYANDO

Washukiwa wawili wa pesa bandia ya Ksh750 milioni wamekamatwa.

Polisi wanaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na washukiwa wawili wa Kenya waliopatikana na pesa bandia Ksh750 milioni.

Wawili hao, Mabw Samuel Maina na Boniface Mungai walipatikana na pesa hizo bandia zilizojazwa kwenye masanduku ya chuma katika sehemu za Kilimani kaunti ya Nairobi.

Pesa hizo zilikuwa katika Dola za Kimarekani, Euro na sarafu ya Kenya.

Polisi waliweza kupata Dola za Kimarekani $6,820,00, Euros 490,000 na Ksh6.4 milioni zote zikiwa bandia.

Kando na hizo pesa bandia, polisi walipata kemikali na beji bandia zilizo na majina ya kambi la UN Della Rue, hazina ya kitaifa na sefu kadhaa za kuweka pesa.

Wapelelezi walisema kuwa wawili hao wanaaminiwa kuwa wakora ambao wanapanga kuwalaghai na kuwapokonya watu na benki pesa kutumia pesa hizo bandia.

[ad_2]

Source link