Home » Waziri Kagwe apiga marufuku safari za ndege kutoka Kenya kuelekea India ▷ Kenya News
News

Waziri Kagwe apiga marufuku safari za ndege kutoka Kenya kuelekea India ▷ Kenya News

Waziri Kagwe apiga marufuku safari za ndege kutoka Kenya kuelekea India ▷ Kenya News

[ad_1]

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kwamba serikali imesitisha safari za ndege kutoka Kenya kuelekea India kwa muda wa siku 14 kwa ajili ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kagwe alisema abiria wote watakaoingia na kutoka nchini kwa sasa watahitajika kupimwa kabla ya saa 72 na wawekwe karantini kwa siku 14.

Aidha, Kagwe amewataka Wakenya ambao watahitaji matibabu nchini India watafuta njia mbadala kwa sababu maambukizi yameongezeka kwa asilimia kubwa.

Kufikia Jumanne, Aprili 28, 2020 India ilikuwa imerekodi visa 360, 960 chini ya saa 24 zilizopita, kwa sasa nchi hiyo imerekodi zaidi ya maambukizi 18 milioni, vifo zaidi ya 200,000.

Source: Tuko Breaking News Latest

[ad_2]

Source link