[ad_1]
Na MASHIRIKA
MSHAMBULIAJI matata raia wa Uruguay, Edinson Cavani, yuko pua na mdomo kukubali ofa itakayomshuhudia akirefusha mkataba wake kambini mwa Manchester United kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.
Cavani, 34, alijiunga na Man-United kwa kandarasi ya mwaka mmoja kutoka Paris Saint-Germain (PSG) ya Ujerumani mnamo Oktoba 2020 huku akiwa na fursa ya kuongezewa miezi 12 zaidi.
Ingawa Cavani alikuwa akihusishwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka ugani Old Trafford na kuingia kambini mwa Boca Juniors nchini Argentina, kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Man-United amefichua kwamba ana azma ya kumshuhudia sogora huyo akisalia kambini mwake.
Licha ya kukabiliwa na panda-shuka tele chini ya Solskjaer kambini mwa Man-United, upo uwezekano mkubwa kwa Cavani kusalia ugani Old Trafford.
Cavani aliwahi kupigwa marufuku ya mechi tatu na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa madai ya kuendeleza ubaguzi wa rangi kupitia ujumbe aliopakia kwenye mtandao wake wa kijamii.
Baada ya kufunga mabao mawili na kuchangia mengine matatu katika ushindi wa 6-2 uliosajiliwa na Man-United dhidi ya AS Roma kwenye mkondo wa kwanza wa nusu-fainali za Europa League muhula huu, Cavani kwa sasa wanajivunia jumla ya magoli 12 kutokana na mashindano yote ya msimu huu.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link









