[ad_1]
Na MASHIRIKA
FOWADI wa zamani wa Brighton na Crystal Palace, Glenn Murray, ameangika daluga zake kwenye ulingo wa soka.
Murray, 37, alijiunga na Nottingham Forest kwa mkataba mfupi mnamo Februari ila akabanduka kambini mwa kikosi hicho mwishoni mwa kampeni za muhula huu wa 2020-21.
Alipachika wavuni mabao 111 kutokana na mechi 285 alizochezea Brighton katika kipindi cha misimu miwili ugani American Express baada ya kuvalia jezi za Palace kwa miaka minne na za AFC Bournemouth kwa mwaka mmoja.
Murray anatamatisha kipindi chake cha usogora baada ya kuhudumu ulingoni mwa miaka 16 huku akijivunia kuwajibikia vikosi mbalimbali vikiwemo Carlisle na Rochdale.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link