[ad_1]
– Siku chache baada ya kifo cha mbunge Kalembe Ndile, jamaa mmoja kutoka kaunti ya Narok amejitokeza na kudai kwamba ni mwanawe
– Stephen Kalembe mwenye umri wa miaka 32 alisema hana haja ya kurithi mali ya babake ila anachokitaka ni kumpa heshima za mwisho
– Kalembe alifariki dunia Jumapili, Mei 30 akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi, anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Mbui Nzau kaunti ya Makueni Ijumaa, Juni 11
Jamaa mmoja ambaye ametambulika kwa majina kama Stephen Kalembe amedai kwamba ni mwanawe marehemu Ndile na angependa kuhudhuria mazishi yake.

Stephen mwenye umri wa miaka 32 alisema kwamba hana haja ya kurithi mali ya babake ila angependa tu kuhudhuria mazishi yake kwa sababu tayari ana mali yake.
” Nishajipanga, nina mali yangu na sitaki kurithi chochote kutoka kwa mali ya babangu, ninachotaka ni kuhudhuria mazishi yake na nimpe heshima zake za mwisho” Stephen alisema
Stephen alisema marehemu Ndile alifahamu vema kwamba alikuwa mwanawe na hakuna vipimo vya DNA vingehitajika kubaini kama kweli alikuwa mwanawe mbunge huyo.
Stephen alisema ni mfanyabiasha ambaye anamiliki mali kadhaa ikiwemo lori na ng’ombe zaidi ya 600.
” Mimi sitaki chochote kutoka kwa babangu, ninachotaka ni kuhudhuria mazishi yake na niweke shahada la maua kwa kaburi lake, nimefanikiwa kwa sababu yake,” Stephen alisema.
Source: Tuko.co.ke
[ad_2]
Source link