[ad_1]
– Duru zinaarifu kuwa baadhi ya watangazaji huo nguli akiwamo Catherine Kasavuli watapamba skrini za runinga ya Shirika la Utangazaji nchini (KBC) kuanzia karibuni
– Kwenye orodha hiyo pia yupo Badi Mukhsin na Tom Mboya ambao wametajwa na chanzo chetu cha ubuyu huu mtamu
Waliokuwa watangazaji wa zamani katika runinga za humu nchini wanatazamiwa kurejea kufanya kazi waliyokuwa wakipenda.
Habari Nyingine: Hawa Ndio Watoto Matajiri Zaidi Ulimwenguni Kufikia Muda Huu, ‘Kuomoka’ kwao Kunatisha

Source: UGC
Duru zinaarifu kuwa baadhi ya watangazaji huo nguli akiwamo Catherine Kasavuli watapamba skrini za runinga ya Shirika la Utangazaji nchini (KBC) kuanzia karibuni.
Ripoti zilizoifikia meza ya haari ya TUKO.co.ke zinasema kuwa, shirika hilo la utangazaji linafanya mabadiliko ya kuboresha na kunogesha kwa kuwaleta nguli ambao kwa kweli waliwachochea wengi wa wanahabari nchini.
Kwenye orodha hiyo pia yupo Badi Mukhsin na Tom Mboya ambao wametajwa na chanzo chetu cha ubuyu huu mtamu.
Habari Nyingine: Wafahamu Mjane wa Marehemu Rais John Pombe Magufuli na Watoto Wao
Source: UGC
Wengi wa watangazaji hao wa zamani walianza kupamba skrini miaka ya themanini wakati Kenya ikingali na televisheni moja tu ambayo ilikuwa ni KBC.
Kasavuli na Muhsin walitangaza pia kwenye redio ya shirika hilo ikiitwa Sauti ya Kenya (Voice of Kenya) na sauti zao pamoja na usogora wao kipindi hicho vilivutia wengi na kufanya runinga hiyo kuangaliwa na wengi.
Habari Nyingine: Birthday Girl Amenitembelea: Ujumbe Mtamu wa Raila Kuhusu Gavana Waiguru
Itakumbukwa kuwa, baada ya kufunguliwa kwa runinga ya KTN, ya kwanza ya mtu binafsi, Kasavuli alifuatwa na kuhamia huko mwaka wa 1990 na wakati wake katika runinga hiyo alijivunia kuwa mtangazaji na mwanamke wa kwanza kusoma habari mbashara.
Baada ya kufanya hapo muda mrefu, Kasavuli alihamia Royal Media Services alipoendeleza kipaji chake licha ya kuwa Meneja wa Kampuni hiyo wa masuala ya Uhusiano kabla ya kustaafu.
Kwa sasa ana miliki Kasavuli Media Group.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Source: Tuko.co.ke
[ad_2]
Source link