Home » Kaunti ya Kisumu yazidi kurekodi visa vingi vya maambukizi ya COVID-19 ▷ Kenya News
News

Kaunti ya Kisumu yazidi kurekodi visa vingi vya maambukizi ya COVID-19 ▷ Kenya News

Kaunti ya Kisumu yazidi kurekodi visa vingi vya maambukizi ya COVID-19 ▷ Kenya News

[ad_1]

– Kaunti ya Kisumu imerekodi visa 100 vipya vya maambukizi ya virusi vya COVID-19 ikifuatwa na kaunti ya Nairobi na visa 91

– Ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo linajiri siku chache baada ya sherehe za siku kuu za madaraka kuandaliwa katika kaunti hiyo

– Visa hivyo sasa vinapelekea jumla ya maambukizi ya virusi hivyo nchini kufikia 173,661 na sampo zilizopimwa kugonga 1,845,884

Visa vya maambukizi ya virusi vya COVID-19 mjini Kisumu vinaendelea kuongezeka wiki moja baada sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya madaraka kuandaliwa mjini humo.

Kaunti ya Kisumu yazidi kurekodi visa vingi vya maambukizi ya COVID-19
Kagwe pia alitangaza kwamba nchi kwa jumla imeripoti visa 589 baada ya sampo 4, 995 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.
Source: Facebook

Kwenye taarifa iliyotolewa na waziri wa afya Mutahi Kagwe, kaunti hiyo imerekodi hii leo Juni 9 visa 100 vya maambukizi ya virusi hivyo ikifuatiwa kwa karibu na kaunti ya Nairobi na visa 99.

Kagwe pia alitangaza kwamba nchi kwa jumla imeripoti visa 589 baada ya sampo 4, 995 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.

Kaunti zingine zikiwemo Bungoma zilirekodi visa 60, Homa Bay 54, Siaya 49, Uasin Gishu 37 Busia 32, Nandi 24, Mombasa 17, Nakuru 17, Kakamega 12, Nyeri 11, Migori 11, Vihiga 9, Kiambu 8, Bomet 7, Meru 7, Kericho 6, Kilifi 6, Kisii 5, na Elgeyo Marakwet visa vitano.

A

Source: Kenyan Breaking News

[ad_2]

Source link