[ad_1]
– Jamaa huyo alivunja nyumba ya ajuza akitambua kwamba mwanawe alikuwa amemuwachia KSh50,000 za ujenzi
– Alimshurutisha bikizee huyo atoe pesa hizo huku akianza kufungua radio na televisheni ili aondoke nazo
– Lakini ajuza alimuomba mwizi huyo ale kwanza kabla ya kuondoka.
– Badala ya kubebea virago alivyompora ajuza huyo na kundoka baada kushiba, alivamia ghafla na usingizi uliomfanya kutiwa mbaroni
Habari Nyingine: Ripoti Zaonesha Marafiki Waliotoweka Kitengela Walihusika na Uhalifu Mombasa
Kulikuwa na kisa cha kutamausha katika kijiji cha Mutomo, kaunti ya Kitui baada ya mwizi sugu wa mabavu eneo hilo kuvamia nyumba ya ajuza mmoja na kisha kulemewa na usingizi.
Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, Jumatatu, Mei 3, mwizi huyo alishindwa kutoroka baada ya kumuibia ajuza na badala yake alikamatwa na usingizi mzito uliomfanya kutiwa mbaroni.
Mwizi huyo alikuwa na mazoea ya kuwahangaisha wanakijiji huku akivamia makazi yao na kuwashurutusha wamupe mali yoyote ya thamani waliyokuwa nayo.
Habari Nyingine: Raphael Tuju Atembea Kilomita 50 kwa Mara ya Kwanza Tangu Kuhusika Kwenye Ajali
Wakati wa siku ya tukio hilo, jamaa huyo alivunja nyumba ya ajuza akitambua kwamba mwanawe alikuwa amemuwachia KSh50,000 za ujenzi.
Alimshurutisha bikizee huyo atoe pesa hizo huku akianza kufungua radio na televisheni ili aondoke nazo.
Lakini ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, ajuza alimuomba mwizi huyo ale kwanza kabla ya kuondoka.
Habari Nyingine: Jamaa Anusurika Kifo Baada ya Mti Kuangukia Choo Alimokuwa Akijisaidia
Na kwa sababu alikuwa anakeketwa na njaa, mwizi huyo alikubali kuketi kitako na kuparamia sahani mbili ya wali iliyokuwa imeandaliwa na bikizee kisha aliitisha maji akate kiu.
Badala ya kubebea virago alivyompora ajuza huyo na kuondoka, alivamiwa ghafla na usingizi kisha alilala.
Akiwa amelala usingizi mzito, polisi waliitwa kwenda kumkamata.
Alipozinduka kutoka usingizini na kuanza kuwekwa pingu alimwambia ajuza huyo: “Kitu gani uliniwekea kwenye chakula? wewe ni nyanya mjanja sana”
Bikizee naye alimjibu: “Ulinioa mzee. Uzee ni mwili, akili ni ya kijana. Nenda tutakutania kortini”
Ajuza huyo alisifiwa na wakazi kwa ujasiri wake wakidai mwizi huyo aliwahangaisha kwa muda mrefu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Source: Tuko
[ad_2]
Source link