Home » Langata: Washukiwa 3 wa Uhalifu Waliokuwa Wamejihami Kushambulia Madereva Wanaswa ▷ Kenya News
News

Langata: Washukiwa 3 wa Uhalifu Waliokuwa Wamejihami Kushambulia Madereva Wanaswa ▷ Kenya News

Langata: Washukiwa 3 wa Uhalifu Waliokuwa Wamejihami Kushambulia Madereva Wanaswa ▷ Kenya News

[ad_1]

– Brian Mwangi na Nickson Muchiri wote wenye umri wa miaka 25 walikamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na maafisa wa polisi kutoka Langata

– Mshukiwa wa tatu mwenye umri wa miaka 15, pia alikamatwa akijaribu kutoroka kupitia Msitu wa Ngong

– Kukamatwa kwao kunakujia kufuatia visa vya mashambulizi dhidi ya madereva kwenye barabara hiyo ya Southern Bypass yenye shughuli nyingi.

Habari Nyingine: Siaya: Rais Uhuru Alipa Karo ya Watoto Maskini Waliomupa Maji Masafi ya Kunywa

Washukiwa watatu waliokuwa wamejihami na panga kuwashambulia madereva kwenye Barabara ya Southern Bypass, walikamatwa Jumapili, Mei 30.

Langata: Washukiwa 3 wa Uhalifu Waliokuwa Wamejihami Kushambulia Madereva Wanaswa
Brian Mwangi na Nickson Muchiri wote wenye umri wa miaka 25 walikamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na maafisa wa polisi kutoka Langata.Picha:Langata.
Source: Twitter

Brian Mwangi na Nickson Muchiri wote wenye umri wa miaka 25 walikamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na maafisa wa polisi kutoka Langata.

Kulingana na taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Jumatatu, Mei 31, mshukiwa wa tatu mwenye umri wa miaka 15, pia alikamatwa akijaribu kutoroka kupitia Msitu wa Ngong.

Habari Nyingine: Nakuru: Kijana Mwenye Umri wa Miaka 17 Aliyekuwa Anajifanya Polisi Akamatwa

Pikipiki mbili ambazo wahalifu hao walikuwa wanatumia kutoroka pia zilipatikana wakati wa operesheni hiyo.

Kukamatwa kwao kunakujia kufuatia visa vya mashambulizi dhidi ya madereva kwenye barabara hiyo ya Southern Bypass yenye shughuli nyingi.

Habari Nyingine: Video Inayoonyesha Helikopta ya Raila Ikiangaka Siaya Yaibuka

Wiki moja iliyopita washukiwa wengine sita walifumaniwa msituni wakati wa operesheni sawia na hiyo baada ya kumshambulia dereva mmoja na mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu.

Washukiwa hao wanatazamiwa kufikiswa kortini hii leo Jumaptatu, Mei 31, kujibu mashtaka ya uhalifu.

Katika taarifa nyingine ya uhalifu, kijana mwenye umri wa miaka 17, ambaye alikuwa anajifanya afisa wa polisi amekamatwa baada ya kunaswa akiwatapeli wateja mjini Nakuru.

Akiwahutubia wanahabari Jumapili, Mei 30, Kamanda wa Polisi wa Nakuru Mashariki Ellena Kabukuru alifichua kuwa kijana huyo alikuwa ameandamana pamoja na mwenzake mwenye umri wa miaka 26.

Wawili hao wanaripotiwa kupatikana na vifaa vya kijeshi ikiwemo pingu na jaketi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Source: Kenya Breaking News Today

[ad_2]

Source link