[ad_1]
Mbunge wa Kaunti ya Omoro Kaskazini mwa Uganda Jacob Oulanuah ameteuliwa kuwa spika wa bunge la 11.
Habari Nyingine: Mpende Msipende, Lazima Waziri Matiang’i Atakuwa Debeni 2022, Mbunge Arama Asema

Source: Getty Images
Habari Nyingine: Wake 2 Wabishania Alikozikwa Mume Wao, Mke wa Kwanza Afukua Mwili
Oulanyah ambaye amechukua nafasi ya spika wa zamani Rebecca Kadaga, aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 310.
Kadaga amekuwa mbunge kwa zaidi ya miongo mitatu na alishikila nafasi ya kuwa spika kwa miaka 10.
Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, chama tawala cha NRM nchini Uganda kilizua mvutano mkubwa kikidai kwamba Kadaga alikuwa ameshikilia wadhifa huo kwa muda mrefu.
Hivyo basi, chama hicho kilimuidhinisha Oulanyah ambaye alikuwa naibu wa Kadaga kuwa spika wa bunge.
Aidha, Kadaga pia aliwania kiti hicho bila kufanikiwa na imeripotiwa kwamba wabunge wanatarajiwa kumchagua naibu wa Spika katika kikao chao cha kwanza ambacho kitafanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Kololo wiki lijalo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Source: Tuko Kenya
[ad_2]
Source link