Home » Mfanyabiashara Chris Kirubi afariki akiwa na umri wa miaka 80 – Taifa Leo
News

Mfanyabiashara Chris Kirubi afariki akiwa na umri wa miaka 80 – Taifa Leo

[ad_1]

Na MWANDISHI WETU

RAIS Uhuru Kenyatta amemwomboleza mfanyabiashara Chris Kirubi ambaye familia yake imethibitisha amefariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 80.

“Nimezipokea habari za kifo cha rafiki yangu Chris Kirubi kwa masikitiko makuu ikizingatiwa kwamba alikuwa mfanyabiashara aliyejitolea kubuni nafasi za ajira kwa maelfu ya watu,” amesema Rais Kenyatta.

Kirubi ambaye amekuwa akiugua kansa, alifanikiwa wakati wa uhai wake kujenga himaya ya biashara ikiwemo kumiliki vyombo vya habari.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha Dkt Christopher J Kirubi (1941-2021), aliyeaga dunia leo, Jumatatu, Juni 14, 2021 saa saba mchana nyumbani kwake baada ya kuugua ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu,” taarifa kutoka kwa familia yake imesema.

Mwaka 2020, Kirubi alifichulia gazeti la Business Daily kuhusu jinsi ambavyo alikuwa akikabiliana na ugonjwa huo.

[ad_2]

Source link