[ad_1]
– Msanii Guardian Angel na Esther Musila wamethibitisha wazi kwamba penzi la dhati lipo na linadumu
– Guardian amemposa Esther kwenye sherehe ya faragha iliyofanyika mtaani Karen jijini Nairobi
– Esther alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na amemshukuru Mungu kwa kutimia umri wa miaka 51
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Guardian Angel hatimaye amemposa mpenzi wake Esther Musila kwenye sherehe nono iliyoandaliwa mtaani Karen jijini Nairobi.
Habari Nyingine: Waziri Fred Matiang’i Atakiwa Kufika Mbele ya Kamati ya Usalama ya Seneti

Source: Instagram
Habari Nyingine: Zogo Lashuhudiwa Katika Bunge la Nyandarua Spika Aliyetimuliwa Alipojaribu Kurejea Afisini
Guardian alisema ili kufanyikisha sherehe hiyo, alimdanganya Esther kwamba walikuwa wanaenda katika shughuli ya kibiashara kusaini dili.
Esther ambaye ametimia miaka 51, alishangazwa baada ya mpenzi wake kumposa wakati alipokuwa akikata keki.
Mama huyo wa watoto watatu alibubujikwa na machozi ya furaha na bila kusita akakubali ombi la mpenziwe.
” Asante sana mpenzi wangu, Aliondoka nyumbani akijua tunaenda kuweka saini kwenye mkataba wa kibiashara lakini ikageuka kuwa Surprise ya kipekee,” Guardian alisema.
Akiwa mwingi wa furaha Esther alisema,” Oh Mungu wangu, nimesema ndio,”
Mashabiki wao mitandaoni wamewatakia heri njema na maisha marefu katika ndoa, TUKO.co.ke iliweza kukusanya baadhi ya maoni;
emmykosgei alisema.”
“Hongera.”
holydavemuthengi alisema:
“Na sisi huku tu ni mchezo, nawatakieni kila la heri mnapoanza ukurasa mpya maishani
stevesnice alisema
“Hongera kaka, wakati wa Mungu ukifika hakuna anayepinga.”
Wapenzi hao wamekuwa wakitusiwa mitandaoni kwa ajili na tofauti kubwa ya umri wao lakini jambo hilo halijazuia penzi lao..
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Source: Tuko
[ad_2]
Source link