[ad_1]
Na SAMMY WAWERU
HUDUMA za afya maeneo ya mashambani katika Kaunti ya Kisumu zinaendelea kuimarika chini ya utawala wa Gavana Anyang’ Nyong’o.
Prof Nyong’o amesema Jumanne, wakati wa maadhimisho ya Madaraka Dei 2021, Kisumu ina hospitali kadha zilizotengenezwa kusaidia kuimarisha huduma za matibabu na afya.
Gavana huyo amesema kina mama wanaojiandaa kujifungua hawahangaiki kupata huduma, kutokana na vituo vya afya vilivyozinduliwa.
“Kisumu ina hospitali kuu ya uzazi nje ya mji, mashambani, ambapo kina mama wanaojifungua kupitia upasuaji husaidika,” akasema Prof Nyong’o.
Alisema serikali ya kaunti yake inaendelea kuweka mikakati maalum kuibuka na vituo kadha vya afya, akilenga kuwa na mojawapo ya hospitali kuu nchini.
Maadhimisho ya Madaraka Dei 2021 yamefanyika katika Kaunti ya Kisumu.
Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla hiyo ya makala ya 58, tangu Kenya ipate uhuru wa kujitawala.
[ad_2]
Source link