Home » Thierry Henry arejea kuwa kocha msaidizi katika timu ya taifa ya Ubelgiji – Taifa Leo
News

Thierry Henry arejea kuwa kocha msaidizi katika timu ya taifa ya Ubelgiji – Taifa Leo

[ad_1]

Na MASHIRIKA

THIERRY Henry amerejea nchini Ubelgiji kushikilia wadhifa wake wa awali wa kocha msaidizi katika timu hiyo ya taifa inayoorodheshwa nambari moja duniani kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Nguli huyo wa Arsenal mwenye umri wa miaka 43 amekuwa bila timu ya kunoa tangu aagane rasmi na kikosi cha Montreal Impact nchini Canada mnamo Februari 2021.

Kwa pamoja na kocha Roberto Martinez, Henry anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika kampeni za Ubelgiji kwenye fainali zijazo za kuwania ufalme wa fainali za Euro zitakazoandaliwa kati ya Juni 11 na Julai 11, 2021.

Henry alikuwa kocha msaidizi kambini mwa Ubelgiji wakati wa fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi na akaongoza kikosi hicho kutinga hatua ya nusu-fainali.

Mwanasoka huyo aliajiriwa na klabu ya AS Monaco mnamo Oktoba 2018 kabla ya kutimuliwa miezi mitatu baadaye kutokana na msururu wa matokeo mabovu.

“Angali na kazi kubwa ya kukamilisha kikosini. Karibu tena Thierry Henry katika benchi ya kiufundi ya timu hii,” ikasema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka la Ubelgiji.

Ubelgiji wametiwa katika Kundi B kwa pamoja na Urusi, Denmark na Finland kwenye fainali za Euro zilizoahirishwa kutoka mwaka wa 2020 kwa sababu ya janga la corona.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]
Source link