Home » Vissel Kobe anayochezea Masika yageuzwa kituo cha kutoa chanjo ya Covid-19 kwa wazee – Taifa Leo
News

Vissel Kobe anayochezea Masika yageuzwa kituo cha kutoa chanjo ya Covid-19 kwa wazee – Taifa Leo

[ad_1]

Na GEOFFREY ANENE

UGA wa Noevir, ambao unatimiwa na klabu ya Vissel Kobe anayochezea Ayub Masika, umeanza Mei 31 kutumiwa kama kituo cha kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa wakazi wa mji mkuu wa jimbo la Hyogo, Kobe.

Vissel ilitangaza kupitia video iliyofanywa na mchezaji wake na shujaa wa Uhispania Andres Iniesta, kuanza kwa zoezi hilo.

Watu walio na umri wa miaka 65 ama zaidi walianza kufika ugani humo asubuhi.

Chanjo zinatolewa katika maeneo ambayo kwa kawaida wageni hawaruhusiwi kufika.

“Chanjo zinapeanwa katika vibanda ambavyo vimewekwa kwenye korido ambazo kwa kawaida hutumiwa na wanasoka,” ripoti hizo zilisema.

Maafisa wanasema kuwa karibu watu 1,000 walitarajiwa katika siku ya kwanza hapo Jumatatu.

“Idadi ya wanaochanjwa inatarajiwa kuongezwa polepole hadi kufikia 5,000 kila siku,” vyombo vya habari nchini Japan vimesema.

Jimbo la Hyogo limeshuhudia visa 55, 510 vya maambukizi ya Covid-19. Jumla ya watu 745,670 wameambukizwa virusi hivyo nchini Japan ambayo imerekodi vifo 12,993.

[ad_2]
Source link