Home » Wamalwa ahusishwa na chama kipya cha DAP-K kilichosajiliwa – Taifa Leo
News

Wamalwa ahusishwa na chama kipya cha DAP-K kilichosajiliwa – Taifa Leo

[ad_1]

Na BRIAN OJAMAA

HUKU siasa za uchaguzi wa 2022 zikiendelea kuchacha, imebainika kwamba chama kipya kinachohusishwa na Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa kimesajiliwa.

Chama hicho Democratic Action Party-Kenya (DAP-K) kilipokea cheti chake kutoka kwa msajili mkuu wa vyama vya kisiasa, Bi Ann Nderitu mnamo Ijumaa.

Pia kinatarajiwa sasa kutoa ushindani mkali kwa Ford Kenya na ANC ambavyo ni maarufu sana katika eneo la Magharibi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.

Mwenyekiti wa chama hicho cha DAP-K ni Bw David Michele kutoka Webuye, Kaunti ya Bungoma.

[ad_2]

Source link