[ad_1]
Na Leonard Owino Onyango
NA MASHIRIKA
NEW YORK, AMERIKA
MKUU wa shirika la kutoa misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa (UN), Mark Lowcock, amesema kwamba maelfu ya watu katika jimbo la Tigray, Kaskazini mwa Ethiopia wanakabiliwa na njaa na kwamba hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Afisa huyo alisema hayo baada ya uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya chakula katika eneo hilo.“Kuna njaa sasa,” alisema na kuongeza kuwa: “ Hali hii itazidi kuwa mbaya.”
Uchunguzi huo ulifichua kuwa watu zaidi ya 500,000 wanaishi katika hali ya mbaya zaidi katika jimbo la Tigray.Tigray limeharibiwa na vita kati ya wanajeshi wa serikali na waasi na watu 1.7 milioni wamefurushwa makwao tangu Novemba 2020.
Kulingana na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa, hali ya njaa katika eneo hilo imefikia kiwango cha janga, kumaanisha kuwa waathiriwa wanakadolea kifo. Kulingana na Umoja wa Mataifa hali ya njaa huwa janga inapoathiri makundi ya watu katika eneo kubwa.
Shirika la Chakula Ulimwenguni, (WFP), Shirika la Chakula na Kilimo, na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto, Unicef, yametoa wito kwa hatua za dharura kuchukuliwa ili kuepuka maafa katika eneo hilo.Serikali ya Ethiopia, haikuidhinisha uchunguzi huo unaofahamika kama
Integrated Phase Classification (IPC) huku ikisisitiza kuwa misaada ya kibinadamu inaendelea kupelekwa eneo hilo.Watu katika wilaya ya Qafta Humera, ambayo imetengwa magharibi mwa Tigray, wiki hii walinukuliwa na BBC wakisema wanakabiliwa na njaa.
Shirika la misaada la Amerika limetuma msaada wa chakula jimbo la Tigray“Hatuna chochote cha kula,” mwanamume mmoja aliambia BBC kwa simu akieleza kuwa mimea na mifugo yao iliharibiwa na kuibwa wakati wa vita vilivyochukua miezi saba.
Mwanamume huyo alisema walizuiwa kutafuta misaada na waasi wanaopigana na wanajeshi wa serikali.’Tulikuwa tunategemea chakula kidogo tulichoficha lakini sasa hatuna chochote,” alisema mkulima mwenye umri wa miaka 40.
“Hakuna aliyetupatia chakula. Karibu kila mtu anakaribia kufariki, macho yetu yameathiriwa na njaa, hali ni mbaya. Kifo kinabisha hodi. Unaweza kuona njaa kwenye nyuso zetu,” alisema.Wakazi wa Magharibi ya Tigray wanasema kwamba mimea yao iliibwa na waasi na chakula kidogo walichoficha kimeisha.
Wanasema kwamba wamekuwa wakiona malori yanayobeba misaada yakipita lakini hakuna aliyewauliza masaibu yao.Mnamo 1984, Tigray na mkoa jirani wa Wollo ilikuwa kitovu cha njaa iliyosababishwa na ukame na vita ambayo ilisababisha vifo vya watu kati ya 600,000 na 1 milioni.
Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa -Integrated Phase Classification- upima kiwango uhaba wa chakula na unahusisha mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa na yasiyo ya kiserikali.
[ad_2]
Source link