[ad_1]
Wizara ya Afya imetangaza kwamba watu wengine 66 wamepatikana na virusi vya COVID-19 baada ya sampo 1, 833 kupimwa chini ya saa 24 zilizopita.

Source: Facebook
Kwa sasa asilimia ya maambukizi ya virusi hivyo kote nchini imetimia 3.6%.
Akihutubua taifa Jumatatu, Mei 10, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kwamba kufikia sasa visa vya maambukizi nchini vimegonga 163, 620 huku jumla ya idadi ya sampo zilizopimwa zikitimia 1,721,122.
Kutokana na visa vilivyoripotiwa kufikia sasa, 65 ni Wakenya ilhali mmoja ni raia wa nchi za kigeni, kijinsia 45 ni wanaume na 21 ni wanawake.
Mgonjwa mdogo ni wa umri wa miaka sita ilhali wa umri wa juu ana miaka 81.
Wagonjwa 1, 737 wamepona kutokana na maradhi hayo chini ya saa 24 zilizopita na kupelekea idadi ya waliopona kufikia 112,298 kwa jumla.
Kulingana na takwimu za wizara ya Afya, wagonjwa 1, 122 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini, 134 wakiwa katika ICU ilhali 4, 783 wakiendelea kupata nafuu manyumbani.
Waziri Kagwe pia alisema jumla ya watu 917,068 wamepokea chanjo ya COVID -19 kati yao 268 walidungwa chini ya saa 24 zilizopita.
Hata hivyo, watu wengine 12 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivi, kwa jumla idadi ya vifo nchini imegonga 2,907.
Source: Tuko Breaking News Latest
[ad_2]
Source link










