[ad_1]
– Kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa Jumanne, Mei 1 katika uwanja wa Jomo Kenyatta, kiongozi wa taifa alionekana akitikisha kichwa chake kwa raha wakati wa kipindi cha burudani
– Hata hivyo wakati nyota wa Benga Osito kalle Kasak alichukua usukuani, kiongozi wa taifa alishindwa kujistahimili na kwa furaha aliinuka alipokuwa ameketi na kuanza kusakata densi
– Viongozi wengine akiwemo Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga na Gavana wa Kisumu Anyang ‘Nyong’o, walijiunga naye kwenye densi
Rais Uhuru Kenyatta aliwafurahisha Wakenya baada ya kusakata densi maarufu ya midundo ya Ohangla wakati wa sherehe ya Siku ya Madaraka huko Kisumu.
Habari Nyingine:
Kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa Jumanne, Mei 1 katika uwanja wa Jomo Kenyatta, kiongozi wa taifa alionekana akitikisha kichwa chake kwa raha wakati wa kipindi cha burudani.
Hata hivyo wakati nyota wa Benga Osito kalle Kasak alichukua usukuani, kiongozi wa taifa alishindwa kujistahimili na kwa furaja aliinuka alipokuwa ameketi na kuanza kusakata densi.
Akiwa amevalia suti nyeusi, shati jeupe na tai nyekundu, Uhuru alipiga viwiko vyake muziki ukiendelea huku akionekana akipiga makofi mara kwa mara.
Viongozi wengine akiwemo Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga na Gavana wa Kisumu Anyang ‘Nyong’o, walijiunga naye kwenye densi.
Waziri Mkuu wa zamani, akitumia mtindo wake wa kucheza alionekana mwingi wa raha wakati mdundo huo ukiendelea ambapo alizunguka mara kdahaa kwenye jukwaa akirusha mikono angani.
Source: Tuko Kenya
[ad_2]
Source link