Home » Uhispania kuvaana na Ureno nao Uholanzi kukutana na Ujerumani nusu-fainali za Euro U-21 – Taifa Leo
News

Uhispania kuvaana na Ureno nao Uholanzi kukutana na Ujerumani nusu-fainali za Euro U-21 – Taifa Leo

[ad_1]

Na MASHIRIKA

UHISPANIA, Uholanzi, Ureno na Ujerumani walifuzu kwa nusu-fainali za Euro kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushinda mechi zao za robo-fainali mnamo Jumanne.

Mabingwa watetezi Uhispania walihitaji muda wa ziada kuwakung’uta Croatia 2-1 huku Uholanzi wakisajili matokeo sawa na hayo dhidi ya Ufaransa.

Ureno waliwapepeta Italia 5-3 katika muda wa ziada huku Ujerumani wakiwabandua Denmark 6-5 kupitia mikwaju ya penalti.

Mechi za nusu-fainali zimepangiwa kupigwa Juni 3, 2021.

Uhispania na Ureno wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la mwaka huu, wanajivunia rekodi ya kutopoteza mechi yoyote hadi sasa, watakutana jijini Maribor, Slovenia.

Ujerumani waliomtegemea pakubwa huduma za kipa Finn Dahmen aliyepangua mikwaju miwili, watakutana na Uholanzi mjini Szekesfehervar, Hungary.

Fainali ya kipute hicho kinachoandaliwa kwa pamoja na Hungary na Slovenia, itachezewa mjini Ljubljana, Slovenia mnamo Juni 6, 2021.

Uingereza walibanduliwa mapema na Croatia kwenye kivumbi hicho katika hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link