Home » Tanzia:Mfanyabiashara tajiri Chris Kirubi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80 ▷ Kenya News
News

Tanzia:Mfanyabiashara tajiri Chris Kirubi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80 ▷ Kenya News

[ad_1]

Mfanyabiashara mkubwa Chris Kirubi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80, familia yake imethibitisha kifo chake.

” Ni kwa huzuni mkubwa kutangaza kifo cha Dkt Christopher J.Kirubi kilichotokea Jumatatu Juni 14 mwendo wa saa saba mchana akiwa nyumbani kwake. Marehemu ameuguaa kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa saratani. Alikata roho akiwa amezingirwa na familia yake,”Taarifa kutoka kwa familia ilisoma.

Tanzia:Mfanyabiashara tajiri Chris Kirubi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80
Kirubi amekuwa akiugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa saratani.Picha: Chris Kirubi.
Source: Facebook

Kirubi ambaye alikata roho Jumatatu, Juni 14, amekuwa akiugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa saratani.

Saa chache kabla ya kifo chake, Kirubi kama ilivyokawaida yake aliwatakia mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter wiki njema yenye fadhila na furaha tele.

” Siku inapoanza, rafiki wangu, haipaswi kuwa Jumatatu ya kuchosha badala yake nakutakia heri njema, fadhila, mafanikio na furaha tele wiki hii mpya. Jipe ratibu ya mafanikio. Furahia siku yako na wiki nzima kwa jumla,” Ujumbe wa mwisho wa Kirubi.

Source: Tuko.co.ke

[ad_2]
Source link